TIMU ya Yanga leo imetimkia Visiwani pemba kwa ajili ya kuanza kambi yao ya kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhi ya watani wao wa jadi Simba, mchezo utakaopigwa Mei 18 kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Wakati Kambi hiyo ikianza leo, Wazee wa klabu ya yanga wametoa tamko juu ya mchezo wa marudiano na watani wao, ambapo wazee hao walianza kutoa pongezi kwa Viongozi wa Klabu ya YANGA chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga kwa kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa mwaka 2012/2013.
Akizungumza kwa niamba ya wazee wenzake Ibrahim Akilimali amesema ubingwa wa yanga umetokana na Uongozi bora, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Klabu na kufikia malengo.
Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani ya Uongozi, wanachama na wachezaji wetu.Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na viongozi na wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013 kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha, shangwe na nderemo.
Sherehe haitakuwepo kama watashindwa kumfunga myama mei 18 uwanja wa taifa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni