TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumanne, 28 Mei 2013

MSANII ALBERT MANGWAIR AFARIKI DUNIA AFRIKA YA KUSINI

Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Msanii mahiri wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwair, amefariki dunia, leo mchana akiwa nchini Afrika ya Kusini.

Chanzo cha habari hizi kimeeleza kwa njia ya SMS kutoka nchini Afrika ya Kusini, kimesema kuwa Msanii huyo amefariki wakati alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Hellena Joseph. 

Aidha Chanzo hicho kimesema kuwa msanii huyo alikuwa akiishi katika Ghetto Moja na Msanii M To The P, ambapo baadhi ya marafiki wa karibu wa msanii huyo walipofika katika geto hilo, walikuta tayari akiwa amefariki huku M To The P, akiwa amepoteza Fahamu ndani ya getho hilo. 
 
Pia Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa Ngwear Huko South Africa.  
Habari zilizo chini ya Kapeti zinasema kuwa Msanii huyo, Mangwair na mwenzake walikuwa wamejidunga madawa ya kulevya na kujioverdose, kiasi cha kuzima na kupoteza fahamu, ambapo wasanii hao walikuwa wakijiandaa kurejea nchini leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni