TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumatatu, 13 Mei 2013

TASWA FC YALALA 2-0 KWA BONGO MOVIE, TASWA QUEENS YAICHAPA BONGO MOVIE 32-10


 Beki na Nahodha wa timu ya Taswa Fc, Mbozi Ernest (kushoto) akiwania mpira na msanii wa Bongo Movie, Vicent Kigosi 'Ray', wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa jana jioni kwenye Viwanja vya TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu ya Bongo Movie, iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Taswa, huku bao la kwanza likifungwa kwa mkwaju wa penati na Ray.
 Wachezaji wa Taswa Queens, wakichuana na wachezaji wa Bongo Movie, wakati wa mchezo wa kirafiki, uliochezwa kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe, jana jioni. Katika mchezo huo Taswa Queens, waliibuka kidedea kwa kuwachapa Bongo Movie jumla ya mabao 32-10.
 Kikosi cha Taswa Fc.
 Kikosi cha Bongo Movie. 
 Sehemu ya mashabiki wa Bongo Movie, waliochanganyika na wachezaji wao wa akiba.
 Wachezaji wa akiba wa Taswa Fc, na wamashabiki wao.
 Mbozi Ernest (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Bongo Movie.
 Mchezaji wa Bongo Movie, Jaqueline Wolper akiruka kudaka mpira wakati wa kipute hicho.
 Kipute kikiendelea......
 Mbozi Ernest (kushoto) akimfinya Stive Nyerere na kumkalisha......
 Duh! wachezaji wa Bongo Movie walikuwa wakicheza kana kwamba wanacheza 'Sini" zao huku wakiwa na Mawigi, Wanja, Ponda na urembo kibao, hapa wigi la mchezaji wa Bongo Movie limeguswa bahati mbaya na kung'oka kichwani.
 Taswa Queens, wakiendelea kutupia.....
 Kipute kinaendelea....
 Gooooooooo.........
 Chiniiiiiiiii, mchezaji wa Bongo Movie akianguka hapa...........
 Ally Mkongwe wa Taswa Fc (kushoto) akivutwa jezi na mchezaji wa Bongo Movie......

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni