TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumanne, 28 Mei 2013

NBC WAMWAGA MISAADA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

Muuguzi  wa  Taasisi ya Saratani  ya Ocean Road  (ORCI) Sr.  Felista John (katikati aliyevaa gauni jeupe) akipokea msaada wa vyakula mbalimbali  kutoka Meneja Uendeshaji Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanaisha Ayosi, iliyotolewa na benki hiyo kitengo cha Operesheni ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo. Wengine ni wafanyakazi katika kitengo hicho.
 Mmoja wa wafanyakazi wa maofisa wa benki ya NBC, Lioba Massao (kushoto) akifanya maombezi kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  (ORCI) katika hafla ambayo benki hiyo kitengo cha operesheni kilikabidhi  msaada wa vyakula mbalimbali ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo na pia kumkabidhi msaada wa sabuni ya kufulia.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakibeba mizigo ya vyakula na mafuta ya kupikia tayari kuwakabidhi wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam kama sehemu ya juhudi za NBC katika kusaidia shughuli za jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni