Rais wa Bendi ya Fm Academia, Nyoshi El-Saadat (kushoto) akipozi na Rais wa Bendi ya Mashujaa, Charz Baba (katikati) na Makamu wa Rais wa Fm, King Braize, wakati wa shoo ya uzinduzi wa Video mpya ya Risasi Kidole ya Mashujaa, uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Green Acres, Victoria jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Nyoshi alimtunuku tuzi Charz na kumvisha ikiwa ni heshima ya kumtambua kuwa Rais wa bendi hiyo akimtakia mafanikio katika kusimamia na kuiendesha bendi hiyo kwa mafanikio.
Wanenguaji wa Bendi ya Mashujaa, wakishambulia mbele ya mashabiki wao wakati wa uzinduzi huo.
Rais wa Fm Academia, Nyoshi (kushoto) akiwangoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa wakati wa uzunduzi huo kwa staili zao 350 walizozitambulisha kati 700.
Sehemu ya Mashabiki wa bendi hiyo, wakifuatilia mashambulizi ya jukwaani.
Wanenguaji wa Mashujaa, wakionyesha shoo yao kali wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Bendi ya Mashujaa, Mama Sakina, akimtunza rapa wa bendi yake Ferguson baada ya kumpagawisha vilivyo kwa rap zake mpya wakati wa uzinduzi huo.
Rais wa Bendi ya Mashujaa, pia alitumia fulsa hiyo kumtambulisha rasmi mchumba wake Rehema Sospeter, kwa kumvisha pete ya uchumba mbele ya mashabiki lukuki waliohudhuria uzinduzi huo.
Mama Sakina akiwa meza kuu na baadhi ya wageni wake waalikwa.....
Fm Academia, wakishambulia jukwaa.................
Mashambulizi ya kusindikiza shoo hiyo kutoka kwa Fm Academi, yakiendelea jukwaani......
Ilikuwa ni zamu ya Nyoshi kuonyesha umahiri wake wa kusebeneka.....
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni