Na VOA
Kufuatia wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu marais Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi yanayopambana na nchi zao, wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya pamoja iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu , wabunge hao wa Kivu Kusini na Kaskazini wameomba kuwe na mtazamo wa jumla wa viongozi wa kanda ya maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini Congo.
Wabunge wa Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa kutaka kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na makundi ya waasi wanayopingana nayo.Wabunge wa Kivu wametaka pendekezo la Rais Kikwete ni lazima lipewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa ili kuwe na amani ya kudumu kwenye eneo hilo.
Mbunge wa upinzani Emerio Kunji kutoka jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa hoja rasmi bungeni ili kuweko na azimio la bunge kuhusu msimamo ambao serikali ya Congo inatakiwa kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu.
Akisema “Rais wa Tanzania alichukua msimamo wa kijasiri wa kuonyesha kwamba mzozo wa maziwa makuu hauwezi kutambuliwa kwa njia ya kinafiki bali kupitia mtizamo ulio thabiti. Bunge letu ni lazima litoe shinikizo kwa serikali ili kuweko na mtizamo mpya wa ufumbuzi wa mzozo huo”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni