TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumatano, 15 Mei 2013

*ROVING KATIKA MITAA YA TABATA LEO


 Waendesha baiskeli za miguu mitatu, 'Guta' wakiwa wamejipumzisha pembezoni mwa njia ya Treni, eneo la Tabata Relini leo mchana bila kujali kuwa eneo hilo ni hatari muda wote.
 Vijana wakichimba mtaro katika Mtaa wa Relini Mwananchi kwa ajili ya kupitisha Bomba la maji ili kusambaza maji hayo ya Kisima kilichochimbwa na Serikali, ili kufikisha huduma hiyo ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo.
 Mtoto huyu kama alivyonaswa na kamera ya Mafoto, haikuweza kufahamika alikuwa akikusanya nini na kuweka katika fuko hili kubwa ambalo baadaye lilionekana kumuelemea wakati wa kubeba, eneo la pembezoni mwa barabara ya Nelson Mandera.
 Hili ni moja ya jengo la Kighorofa lililopo pembezoni mwa barabara ya Mandera, ambalo siku za nyuma inaonekana ndilo hasa lilikuwa kivutio katika eneo hili... 
 Boda boda nazo siku hizi pamoja na kuogopwa na baadhi ya watu kwa kujihusisha na uharifu, lakini bado zimezidi kuongezeka kila kona ya mitaa ya jijini Dar es Salaam, hapa wakiwa katika kituo cha daladala wakisubiri abiria. 
 Barabara ya Mandera mida ya mchana na jioni kumekuwa na foleni kubwa siku zote kiasi cha kusababisha magari mengine kuvunja sheria za usalama barabarani na kupita katika njia 'Service Road', pichani baada ya Service road kujaa, gari hilo lililokuwa na askari Magereza na raia ambao haikuweza kufahamika kuwa walikuwa ni watuhumiwa ama la, likipita kwa taabu pembeni mwa magari mengine huku likiwa limewasha taa kuashiria dharura, laikini bado magari yalishindwa kulipisha.
Askari wa usalama Barabarani, wakiwakamata madereva wa magari yaliyokuwa yakipita katika Service Road baada ya barabara zote kujaa magari na kuwaandikia kulipa faini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni