TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumapili, 20 Oktoba 2013

SIMBA ILIPOWASHANGAZA MASHABIKI WA SOKA JANA,ILIPOCHOMOA MABAO 3 NA KULAZIMISHA SARE YA 3-3

 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akiwania mpira na kipa wa Simba Abel Dhaira, wakati wa kipindi cha pili cha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 3-3, ambapo Yanga ilipata mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa wachezaji Mrisho Ngasa, aliyetupia katika dakika ya 15, Hamis Kiiza 36 na 45. 

Mabao ya Simba yalifungwa kipindi cha pili kupitia wachezaji wake, Betram Mwombeki, katika dakika ya 54, Joseph Owino katika dakika ya 57 na Gilbert Kaze, katika dakika ya 83. 
Baada ya Simba kusawazisha mabao yote matatu viongozi na mashabiki wa timu hiyo walionekana kushangilia sare hiyo, ambayo kila mmoja aliyekuwapo uwanjani hapo hakuweza kuamini kilichotokea kuanzia mashabiki, wachezaji wa Yanga na hata wa Simba.
 Mashabiki wa Simba, walikuwa kama wamemwagiwa maji, wakiwa na huzuni katika kipindi cha kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0.
 Mshambuliaji Mrisho Ngasa, (kulia) akimtoka beki wa Simba, Joseph Owino, katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kulia) akiwatoka mabeki wa Simba, Joseph Owino na Gilbert Kaze, katika kipindi cha kwanza.
 Mrisho Ngasa, akiruka kwanja la beki, Gilbert Kaze.
 Mashabiki wa Yanga ilikuwa ni furaha kama hivi, ambapo baadaye furaha hii ilizimika ghafla.
 Katika mtanange huo, mashabiki kadhaa walizimia, ambapo shabiki huyu wa Yanga, akibebwa kutoka jukwaani baada ya kuzimia, huku mashabiki saba wa Simba na wawili wa Yanga walizimia.
 Mshabiki wa Simba walizinduka na kushangweka kama hivi, baada ya kupata bao la pili.
Mrisho Ngasa, akishangilia bao lake la kwanza alilofunga katika dakika ya 15, kipindi cha kwanza.

Jumamosi, 7 Septemba 2013

*UBINAFSI/UFISADI WA MENGI NA CHUKI/FITINA KWENYE MAENDELEO.

Hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watanzania dhidi ya Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Prof Sospeter Muhongo yakiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambae pia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bwana Reginald Mengi. Malalamiko hayo ambayo yameendelea kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari na kupelekea hata baadhi ya wahusika kutoka wizarani, Idara na Mashirika yake kutakiwa kujibu na kutolea ufafanuzi malalamiko na tuhuma hizo nzito dhidi yao. Moja ya vyombo hivyo ni gazeti la NIPASHE linalomilikiwa na IPP media la tarehe 6 septemba, 2013 katika ukurasa wake wa tatu kuna habari inasema “SERIKALI YAZIDI KUPUUZA USHAURI WA TPSF” Inaeleza habari hiyo kuwa “ ..Wakati taasisi ya sekta binafsi (TPSF) ikiishauri kuharakisha sera ya gesi badala ya ugawaji vitalu, serikali imeendelea kupuuza ushauri huo na sasa kupitia Shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) imetangaza rasmi kuharakisha suala hilo kwa madai ya kuwahi ushindani wa masoko ulimwenguni..”

Lakini TPDF nao katika gazeti la UHURU la jana Ijumaa katika ukurasa wake wa tatu imeandikwa habari yenye anuani “MWENYEKITI TPDC: UBINAFSI UNAWAPONZA WATANZANIA. ->wengi wanalalamika uwezo hawana,
-> Zabuni za vitalu mwezi ujao.” katika habari hiyo Mwandishi ameandika kuwa “Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) , Michael Mwanda, amesema ubinafsi miongoni mwa watanzania ndio unaowafanya washindwe kunufaika na fursa za kiuchumi zilizopo nchini, zikiwemo mafuta na gesi. Mwanda alisema hayo jana jijini Dar es salaam, alipokuwa akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari juu ya malalamiko ya baadhi ya watanzania kuwa hawapewi nafasi kushiriki katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.”

Malumbano hayo kupitia vyombo vya habari baina ya pande mbili yaani Mengi na IPP yake na Muhongo na Mashirika yake ambayo yamedumu kwa muda, sasa yanachukua sura mpya baada ya kuwepo kwa taarifa za chini chini kuwa Mwenyekiti huyo wa TPSF na IPP ameandaa mpango wa kuwatumia vijana wa Chama Cha Siasa cha Upinzani (CHADEMA) kufanya kongamano lenye maudhui “rasilimali za nchi na manufaa kwa wazalendo” ambapo kongamano hilo limepangwa kupewa airtime katika kituo maarufu cha television hapa nchini cha ITV ambacho kinamilikiwa na IPP media lakini pia posho, chakula na incentives mbalimbali zimepangwa kutolewa katika Kongamano hilo.

Kama ilivyo katika mkakati huo, lengo lililopo nyuma ya pazia la kongamano hilo ni kutaka kuionyesha jamii kuwa Waziri na Wizara kwa ujumla haijali maslahi ya wazawa na kwamba viongozi wakuu wa Wizara husika hawana Utaifa wala Uzalendo (kwa maana ya upendo kwa Taifa) hivyo wanataka kuzitumia nafasi zao ndani ya wizara katika kujitajirisha binafsi na kufanya upendeleo kwa wawekezaji wageni ambao hawana manufaa ya moja kwa moja katika maendeleo ya wananchi.

Madhumuni ya andiko langu hili na kuvuta utafakari makini na wa wengi katika suala hili ambalo kama hatua muhimu na za haraka hazitachukuliwa katika kulikabili linaweza kuleta tafsiri hasi kwa jamii na hivyo kuwagawa na kuwavuruga watanzania na hasa kuwafanya wapoteze imani na matumaini yao kwa Serikali, Waziri, Wizara, Idara na Mashirika yaliyopewa dhamana ya usimamizi wa rasilimali za nchi hii.

Naomba ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza kwa seke seke la aina hii kuzuka ama kuzushwa chini ya uratibu na usimamizi wa Mzee Mengi. Na mara zote amekuwa akitumia nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habari anavyovimiliki katika kutafuta kuungwa mkono na hata kuonyesha ubaya wa wabaya wake. Ubaya, malumbano na mizengwe mingi ambayo huzalishwa na kusimamiwa na Mzee wangu huyu asili yake ni Ubinafsi na kuguswa kwa maslahi ya kiuchumi aliyonayo katika Sekta mbalimbali hapa nchini.

Hivi karibuni kulizuka sekeseke mfano wa hili la sasa ambalo lilihusu VING'AMUZI na kabla ya hapo TBC, UBINAFSISHAJI WA KILIMANJARO HOTEL, SUALA LA YUSUPH MANJI, SHEIKH AL BASALEHE na katika migogoro yote hiyo Mzee Mengi amekuwa akitumia vyombo vya habari katika kuwakandamiza, kuwazushia, kuwatuhumu na hata kuwadhalilisha wapinzani wake. Nitaomba wanajamvi wakumbuke kuwa Mwaka 2008 kulipokuwepo mgogoro baina ya Mzee Mengi na Al Basalehe, Katika mgogoro huo Mzee mengi alimrubuni Ustadhi Mmoja wa madrasa (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) na kuwatumia wanafunzi wa madrasa hiyo kutunga nyimbo za kaswida za kumdhalilisha Sheikh Al Basalahe na kisha nyimbo hiyo kupewa airtime katika kituo cha ITV, na kwa mfano kama huo akaitumia ITV kuwataja washindani wake kiuchumi kuwa ni MAFISADI PAPA.
Sina kumbukumbu kuwa alitumia vigezo gani kuwataja wapinzani wake hao kibiashara kama mafisadi papa, ila kumbukumbu yangu inaniambia aliwataja hadharani na kupelekea baadhi kumpeleka mahakamani na kumfungilia kesi ambazo hata hivyo hazikupata airtime za kutosha kwenye vyombo vya habari na hata mwisho wake haukuwa umefahamika kwa wengi.

Tukirudi katika hoja yetu ya vitalu vya gesi ambavyo Mwenyekiti huyo wa IPP na TPSF amekuwa akividai kwa hamu kubwa na kuwatuhumu Viongozi wa Wizara, Wakuu wa Idara na Mashirika yanayohusu Rasilimali gesi na mafuta kuwa hawana hata chembe ya Uzalendo na wabinafsi, nahofu nitaeleweka vibaya kwa baadhi ya watu nikisema kuwa kauli hii haina uhalisia na si ya kweli, na kwamba inalenga kuchochea hisia za chuki na imetolewa kwa misingi ya Chuki, it's simply a hate speech that hate are produced.

Kwa mujibu wa TPDC, kuchimba kisima kimoja kwa ajili ya kutafuta gesi na mafuta katika nchi kavu ni dola za Marekani milioni 40 (Tshs. Bilioni 64) na kwa kina kirefu cha bahari ni dola 120 (Tshs Bilioni 190) na pia ili kupata mafuta au gesi baada ya kupata uhakika, mwekezaji anapaswa kuchimba visima vinne hadi vitano, hivyo inahitaji mwekezaji kuwa na mtaji usiopungua dola za kimarekani milioni 600 ~ 800 kiasi ambacho watanzania wengi hawana (MENGI akiwemo) na kwa Kauli ya Mwanda, Mwenyekiti wa TPDC alisema kuwa Watanzania ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo, hawana budi kuungana na wabia wenye uwezo wa kimtaji na teknolojia (Suala ambalo Mengi analipinga)

Tatizo la kimsingi hapa ni Ubinafsi wa baadhi ya watu ambao wanataka upendeleo kwa maslahi binafsi ya kibiashara kwa nembo ya uzalendo na uzawa. Kumekuwepo na rekodi zenye kusikitisha ambazo zinaonyesha tatizo la msingi linalowakabili hawa tycoon wetu katika mikopo waliyochukua katika mabenki makubwa mbalimbali hapa nchini na hata nje ambapo bado hawajarejesha mikopo hiyo na hivyo kutokopesheka tena kwa miradi mikubwa kama hii ya vitalu vya gesi lakini pia zipo rekodi nyingine zinazoonyesha wametumia mikopo kwa shughuli ambazo hawakuombea mikopo hiyo ikiwemo mikopo kutoka benki ya kilimo (Takwimu zipo)

Kama hayo ya mikopo hayatoshi, tayari Kampuni za Mzee Mengi zinashikilia vitalu takribani 59 vya madini vyenye Ukubwa wa mita za mraba 3,752. 37 (sq km) na baadhi ya vitalu hivyo alivyovishikilia ameshindwa kuviendeleza na matokeo yake Serikali inakosa mapato kutokana na kutoendelezwa kwa vitalu hivyo lakini pia watanzania wanakosa ajira na manufaa mengine, najiuliza kama hii ndio tafsiri ya UZAWA ambayo Mzee Mengi anaizungumza, ama ni AINA nyingine ya UFISADI ambayo watanzania walio wengi bado hawajaung'amua kwa kuwa vyombo vya habari haviandiki wala kusema kuhusu habari hizi. Katika attachment ni orodha ya vitalu mbalimbali vinavyomilikiwa na Kampuni za Mzee Mengi hapa nchini.

Tunaweza kutofautiana katika mengine lakini katika yale yanayohusu mustakabali wa nchi naomba watanzania tuungane na tuseme hapana. Matumizi ya Vyama vya Siasa, wanasiasa na hata pressure group katika kutetea maslahi ya baadhi ya tycoon wa hapa nchini ni hata nje ni katika makosa makubwa ambayo yanaweza kutuletea madhara makubwa sana hasa kutokana na rasilimali zilizopo hivi sasa hapa nchini. Nitoe ombi kwa Vijana hawa wa Chadema, watambue nafasi yao kama vijana na Safari waliyonayo ya kuijenga kesho yao na kusahau posho za siku moja na vyakula. Ni wakati wa kusimamia haki na kuitetea kweli, hata ikiwa kweli hiyo inakinzana na maslahi binafsi.

Jumatano, 31 Julai 2013

Wavutaji Sigara wa Jijini Nairobi wanavyodhibitiwa kutovuta hovyo sigara mtaani

Baadhi ya wavutaji wa sigara wakiwa katika chumba kimoja katijati ta  jiji la nairobi wakivuta sugara kutokana na nchi ya kenya kuweka msimamo na kusimamia sheria ya kutovuta sigara katika eneo lenye watu wengine wasiotumia sigara. jambo hilo humfanya mtu kutembea umbali mrefu kutafuta eneo hilo maalum kwa uvutaji wa sigara tofauti na nchi nyinginezo mnapishana tu na wavutaji tena wakikupulizia moshi usini.

Jumapili, 28 Julai 2013

ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYANI KARAGWE

 Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo.
 Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo.
 Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013.

Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara.
 Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013.

*BALOZI SEIF IDDI AKUTANA NA VIJANA WA HATUDANGANYIKI MKOA WA KASKAZINI PEMBA LEO

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akizungumza na Vijana wa CCM wa Kikundi cha Hatudanganyiki cha Mkoa wa Kaskazini Pemba kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jamuhuri Wete Kisiwani Pemba.
 Balozi Seif akiwafariji Ndugu na Jamaa wa Mwanaharakati wa Chama cha Mapinduzi Chake chake Pemba Marehemu Fatma Omar Khatib aliyefariki Dunia hivi karibuni baada ya kugongwa na gari Mjini Chake.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akisalimiana, kumkagua hali na kubadilishana nae mawazo mwanaharakati wa Chama cha Mapinduzi Bibi Habiba Ali Hamadi nyumbani kwake mtaa wa Michakaeni Chake chake Pemba.
Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika harakati za kuwakagua na kuwapa pole wanaharakati wa chama cha mapinduzi Chake chake Kisiwani Pemba waliopatwa na misiba pamoja na ajali hivi karibuni. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
**********************************
Mjumbe wa  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi amekemea tabia ya baadhi ya Viongozi wa Chama hicho kuwa na hulka ya kuwatenga Vijana ambao ndio muhimili na wenye nguvu katika kukipigania Chama hicho.
Kauli hiyo aliitoa katika Ukumbi wa Jamuhuri Wete Pemba wakati akizungumza na vijana wa Chama cha Mapinduzi wa kikundi cha Hatudanganyiki mara baada ya kupokea malalamiko yao dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama hicho Wilaya ya Wete na Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema zipo kasoro ndogo ndogo zinazotofautiana za mawazo zilizopo baina ya Viongozi na Wanachama lakini  haziwezi kuachwa zinaendelea kudhoofisha nguvu za Chama hicho.
Aliwaasa wana CCM hao kujiepusha na mgawanyiko ndani ya chama ambao unaweza kuleta balaa na kitu kinachowakabili hivi sasa  mbele yao ni kuhakikisha wanapanga mikakati katika kuimarisha nguvu ya chama chao kwa ajili ya ushindi wa mwaka 2015.
Alitahadharisha kwamba hitilafu zinazojichomoza baina ya Viongozi na Wanachama wa chama hicho ni vyema zikatatuliwa na kuishia katika Vikao vya halali na kujiepusha na tabia ya kuitana majina ya ajabu ambayo hutoa mwanya wa kudhoofisha chama.
Balozi Seif alielezea kuunga mkono  vijana hao wa CCM wa kundi la hatudanganyiki Kaskazini Pemba kwa ushujaa wao wa kutetea na kuimarisha Chama cha Mapinduzi na Kuuagiza Uongozi wa CCM Wilaya ya Wete pamoja na Mkoa wa Kaskazini Pemba kufuatilia matatizo yanayowakabili Vijana hao na hatimae kuyatatua nay ale wasio na uwezo nayo kuyawasilisha kwa Uongozi wa Juu wa Chama.
“ Mimi kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambae pia nasimamia shughuli za Serikali ya Chama Tawala nitahakikisha baadhi ya matatizo yenu Vijana nayawasilisha kwa Makamu Mwenyekiti wetu wa CCM Zanzibar ili itafutwe mbinu ya kuyatatua “. Alisisitiza Balozi Seif.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwapongeza wana CCM Kisiwani Pemba kwa msimamo wao wa kuendelea kukiunga mkono chama hicho.
Alisema Wanachama wa chama hicho Kisiwani humo ni madhubuti kutokana na kutoyumba kwao licha ya mikiki mikiki wanayopambana nayo kutoka kwa kambi ya upinzani hasa katika nyakati za uchaguzi.
“ Ushindi wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu unategemea sana wana CCM wa upande wa Kisiwa cha Pemba ambao hawatetereki wala kuyumba kutokana na vitisho vya upinzani “. Alisisitiza Balozi Seif.
Balozi Seif aliendelea kufahamisha kwamba nguvu na uhai wa Chama cha Mapinduzi mara zote unategemea jumuiya zake za Wazazi, Vijana na UWT, hivyo  Vijana hao wanapaswa kuelewa kwamba wao ni tegemeo la Chama wakati wote.
Mapema Vijana hao wa CCM wa kikundi cha hatudanganyiki wakiongozwa na Mwenyekiti wao Omar Rashid walielezea changamoto wanazokabiliana nazo kila siku katika harakati zao za kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Walisema asilimia kubwa ya changa moto hizo ambazo zimo ndani ya uwezo wa Viongozi wenyewe zimekuwa zikiwapa wakati mgumu kutokana na udhaifu binafsi uliopo kwa baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa.
Walieleza kwamba upo ushahidi wa wazi unaoonyesha baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya na Mkoa kufuja mali za Chama kwa maslahi yao binafsi pamoja na kujishirirkisha katika vitendo vya rushwa wakati zinapotokea fursa za ajira kwa ajili ya Vijana hao.
Baadaye Balozi Seif alifika katika Kijiji cha Michakaeni Chake Chake Pemba kuipa pole Familia ya Mwanaharakati wa Chama cha Mapinduzi Marehemu Bibi Fatma Omar Khatib ambae aliyefariki dunia hivi karibuni baada ya kupata ajali ya kugongwa na Gari.
Akiifariji Familia hiyo Balozi Seif aliwataka ndugu na jamaa wa marehemu Bibi Fatma Omar Khatib kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Alisema msiba huo wa Bibi Fatma ambao utaendelea kukumbukwa katika kipindi kirefu mbali ya kuiathiri familia hiyo lakini pia umewagusa takriban wana chama wa chama cha mapinduzi wote waliopata taarifa ya msiba huo Zanzibar na bara kwa ujumla.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM pia alimtembelea Mzee mwanaharakati wa CCM wa miaka mingi Kisiwani Pemba Bibi Habiba Ali Hamadi hapo nyumbani kwake Mtaa wa Michakaeni.
Bibi Habiba mwenye umri wa Miaka 70 aliwahi kupata ajali ya gari wakati wa kampeni za mwanzo za uchaguzi wa vyama vingi vya siasa ambapo CCM iliibuka na ushindi kwa kumuwezesha Dr. Salmin Amour kuiongoza  Zanzibar mnamo mwaka 1995.
Balozi Seif alimuahidi Bibi Habiba ambae hadi sasa ni Balozi wa CCM wa nyumba kumbi kwamba Uongozi wa chama cha Mapinduzi utakuwa pamoja na  yeye kwa kumpatia misaada kadri hali itakavyoruhusu kutokana na mchango wake mkubwa aliyoitoa ndani ya chama hicho.
 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/7/2013

Jumamosi, 20 Julai 2013

*MIILI YA ASKARI WALIOKUFA DARFUR YAWASILI NCHINI LEO JIONI, MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AONGOZA MAPOKEZI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni. 
Na www.sufianimafoto.com
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. 

Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi.

Mbali na Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, ni pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete.

Mara baada ya kuwasili miili hiyo iliongozwa na msafara kuelekea hospitali ya rufaa ya Jeshi,  Lugalo, kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi siku ya Jumatatu Julai 22, 2013 itakapoagwa rasmi kwa heshima zote katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es Salaam, ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi Mkabala na Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.

Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni.
 Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
 Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur.
 Baadhi ya wananchi waliofika kupokea na kushuhudia mapokezi  hayo ya miili ya mashujaa wetu.
 Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
 Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akishikiliwa na wenzake wakati akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
 Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima.
 Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
 Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo.

Jumapili, 7 Julai 2013

*Crash landing at San Francisco airport kills 2

SAN FRANCISCO (AP) — An Asiana Airlines flight packed with more than 300 people slammed into the runway while landing at San Francisco airport Saturday and caught fire, forcing many to escape by sliding down the emergency inflatable slides as flames tore through the plane.
At least two people died in the crash, while another 181 people were taken to hospitals, most with minor injuries, authorities said. Five people, including one child, remained in critical condition at San Francisco General Hospital, the region's main trauma center.
As the plane approached the runway from the waters of San Francisco Bay around noon, travelers in the terminals and others eyewitnesses could see that the aircraft was swaying unusually from side to side and that at one point the tail seemed to hit the ground.
Kate Belding, who was jogging a few miles away, said she thought: "Oh my God. That plane is crashing."
By the time the flames were out, the top of the Boeing 777's fuselage had burned away. The tail section was gone, with pieces of it scattered across the beginning of the runway. One engine appeared to have broken away. Emergency responders could be seen walking inside the burned-out wreckage.
News of the crash spread quickly on Twitter and the Internet in this wired city, with eyewitnesses tweeting their stories, posting images of the plumes of smoke rising above the bay and uploading video of passengers fleeing the burning plane.
"It just looked really bad," Belding said. "I've seen the pictures of it since then, and it's amazing anyone walked out of that plane."
The investigation has been turned over to the FBI and terrorism has been ruled out, said San Francisco Fire Chief Joanne Hayes-White said. Federal aviation and transportation investigators were heading to the scene. Asiana, Boeing and the engine manufacturer, Pratt & Whitney, pledged to work with them.
Vedpal Singh, who was sitting in the middle of the aircraft and survived the crash with his family, said there was no forewarning from the pilot or any crew members before the plane touched down hard and he heard a loud sound.
"We knew something was horrible wrong," said Singh, who suffered a fractured collarbone and had his arm was in a sling.
"It's miraculous we survived," he said.
A visibly shaken Singh said the plane went silent before people tried to get out anyway they could. His 15-year-old son said luggage tumbled from the overhead bins The entire incident lasted about 10 seconds.
Based on witness accounts in the news and video of the wreckage, Mike Barr, a former military pilot and accident investigator who teaches aviation safety at the University of Southern California, said it appeared the plane approached the runway too low and something may have caught the runway lip — the seawall at the end of the runway.
San Francisco is one of several airports around the country that border bodies of water that have walls at the end of their runways to prevent planes that overrun a runway from ending up in the water.
Since the plane was about to land, its landing gear would have already been down, Barr said. It's possible the landing gear or the tail of the plane hit the seawall, he said. If that happened, it would effectively slam the plane into the runway, he said.
Noting that some witnesses reported hearing the plane's engines rev up just before the crash, Barr said that would be consistent with a pilot who realized at the last minute that the plane was too low and was increasing power to the engines to try to increase altitude. Barr said he could think of no reason why a plane would come in to land that low.
Belding was out jogging just before 11:30 a.m. on a path across the water from the airport when she noticed the plane approaching the runway in a way that "just didn't look like it was coming in quite right."
"Then all of a sudden I saw what looked like a cloud of dirt puffing up and then there was a big bang and it kind of looked like the plane maybe bounced (as it neared the ground)," she said. "I couldn't really tell what happened, but you saw the wings going up and (in) a weird angle."
"Not like it was cartwheeling," she said, but rather as though the wings were almost swaying from side to side.
The flight originated in Shanghai, China, and stopped over in Seoul, South Korea, before coming to San Francisco, airport officials said. The airline said there were 16 crew members aboard, and the 291 passengers included 77 South Koreans, 141 Chinese, 61 Americans and one Japanese citizen. The nationalities of the remaining passengers weren't immediately known.
Airport spokesman Doug Yakel said 49 people were in serious condition and 132 had less significant injuries.
The airport closed for several hours, and when it reopened, two of the four runways were operating.
Asiana is a South Korean airline, second in size to national carrier Korean Air. It has recently tried to expand its presence in the United States, and joined the Star Alliance, which is anchored in the U.S. by United Airlines.
The 777-200 is a long-range plane from Boeing. The twin-engine aircraft is one of the world's most popular long-distance planes, often used for flights of 12 hours or more, from one continent to another. The airline's website says its 777s can carry between 246 to 300 passengers.
The flight was 10 hours and 23 minutes, according to FlightAware, a flight tracking service. The 777 is a smaller, wide-body jet that can travel long distances without refueling and is typically used for long flights over water.
The most notable accident involving a 777 occurred on Jan. 17, 2008 at Heathrow Airport in London. British Airways Flight 28 landed hard about 1,000 feet short of the runway and slid onto the start of the runway. The impact broke the 777-200's landing gear. There were 47 injuries, but no fatalities.
An investigation revealed ice pellets that had formed in the fuel were clogging the fuel-oil heat exchanger, blocking fuel from reaching the plane's engines. The Rolls-Royce Trent 800 series engines that were used on the plane were then redesigned.
Bill Waldock, an expert on aviation accident investigation, said he was reminded of the Heathrow accident as he watched video of Saturday's crash. "Of course, there is no indication directly that's what happened here," he said. "That's what the investigation is going to have to find out."
The Asiana 777 "was right at the landing phase and for whatever reason the landing went wrong," said Waldock, director of the Embry-Riddle Aeronautical University accident investigation laboratory in Prescott, Ariz.
"For whatever reason, they appeared to go low on approach and then the airplane pitched up suddenly to an extreme attitude, which could have been the pilots trying to keep it out of the ground," he said.
The last time a large U.S. airline lost a plane in a fatal crash was an American Airlines Airbus A300 taking off from John F. Kennedy International Airport in New York in 2001.
Asia remains one of the fastest-growing regions for aviation in the world. Even with slowing economies in Japan and China, airlines there saw 3.7 percent more passengers than a year ago, according to the International Air Transport Association.
Finding enough experienced pilots to meet a growing number of flights is becoming a problem. A 2012 report by aircraft manufacturer Boeing said the industry would need 460,000 new commercial airline pilots in the next two decades — with 185,000 of them needed in Asia alone.
"The Asia-Pacific region continues to present the largest projected growth in pilot demand," the report said.
"