TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumatano, 15 Mei 2013

MUZIKI GANI WA DIAMOND PLATNUMS NA NAY WA MITEGO NANI MKWELI ZAIDI? PATA MASHAHIRI KAMILI


 Diamond Platnums na Nay wa Mitego wakiwa Studio wakati wakirekodi wimbo wao wa Muziki gani.


UNAJISIKIA burudani kila unapokuwa ukiusikiliza wimbo huu wa 'Muziki Gani' ambao ni kolabo kati ya Ney wa Mitego na Diamond, walioamua kuimba kwa pamoja huku kila mmoja akielezea mapungufu na ukweli wa maisha ya kimuziki ya mwenzake.

Ama kwa hakika unaweza kuhisi kuwa jamaa hawa hawakuingia katika studia moja na kufanya kazi hii kwa pamoja, pindi tu unapousikiliza wimbo huu unaweza kuhisi kuwa kila mmoja aliandika mashahiri yake kivyake na kisha akaingia studio kila mmoja kwa wakati wake na kisha wakamuachia kazi Producer ili kuunganisha, lakini si kweli, ila wakali hawa walichukua maamuzi magumu na ya busara.Maamuzi haya yaliyochukuliwa na wakali hawa yalikuwa ni kila mmoja kufunga masikio na kujifanya hasikii maneno yaliyokuwa yakiimbwa namwenzake, kisha klazi ikaenda na sasa imekuwa bomba na gumzo midomoni mwa mashabiki wa muziki huu wa Bongo Flava.

Haikuweza kufahamika sababu za wasanii hawa kukaa pamoja na kuimba song hili kwa pamoja, kwani mtandao huu uliweza kumtafuta Diamond kwa njia ya simu ambaye muda wote hakuwa akipokea simu na badala yake alikuwa akipokea mdada aliyetambulika kwa jina la Halima Kimwana, ambaye pia hakutaka kujitambulisha kuwa ni nani kwa Diamond, ambapo mdada huyo alisema kuwa ''kama unataka kufanya mahojiano na Diamond, amesema uongee na mimi''. mwisho wa kunukuu.

Kwa upande wa Nay, hakuweza kabisa kupatikana kutokana na kukosekana kwa namba yake ya simu ya mkononi, ambapo aliyetakiwa kutoa ushirikiano na mtandao huu ni Msanii Shetta, ambaye naye kila alipopigiwa alionyesha kuwa bize. 

Hii pia ni moja ya sababu zinazosababisha kuporomoka kwa wasanii wanaovuma kama Diamond, kwani mifano iliyo hai ni mingi tu, mmoja wapo ni Msanii Mr Nice, japo yeye hakuwa na 'dharau zilizokithiri'  kama wenginee.

SONG LINAANZA,.....PATA FLAVA...KUTOKA KWA NAY NA DIAMOND
Diamond:- Q-Ssss
Nay:- Ludboooy, Sadactive Records, Ludboooy,Your Beatfull Beibeeeee, Ludboooyyyyy
Wasaaafii

CHORUS:- Diamond
Hivi Nyie Ma Mc's.... Mnachoimba kitu ganii, mara Bange mara Matusi sa ndo muziki ganii....

CHORUS:- Nay
Hii ni HIP HOP H.O.P, Ludboooy, Mwasisi wa burudanii, aah!, ukishatosha kutoa mapenzi kabane pua nyumbaniii....

CHORUS:- Diamond
Hivi Nyie Ma Mc's Mnachoimba kitu ganii, mara Bange mara Matusi sa ndo muziki ganii,

CHORUS:- Nay
Hii ni HIP HOP H.O.P, Ludboooy, Mwasisi wa burudanii, aah!, ukishatosha kutoa mapenzi kabane pua nyumbaniii

DIAMOND:-
Hata Bibi yangu me aliniambia, Mwanamke anahitaji kubembelezwa, Kupetipeti matunzo pia, Ukienda rafu utampoteza, Muziki ni mfano wa Binti Muzuurii..., Na Ndo maana namtunza kwa vazi la uturiii.....

NAY:- A, aah!! Piga kimya, We ndo haufai kabisaa, Hauna Maana, Wabana pua kila siku mnalogana, Bibi yako alikuambia muziki ni kama Binti mbona unawachezea unawatema kama Big Jii,....Mara  Wema, Mara Joket, Mara Nargis, Mara Penny, Je mnafanya muziki ili mpate mabinti????

Diamond:- Uuu, uuuhhh!! Hata wazee wa zamani, walishasemaga kazi na dawa, Cha muhimu Jukwaani ni kuhakikisha wanapagawaa, Kwa michezo ya kuringa ringaa, ndo huwa wanadataaaaa, Badilika usiwe mjinga, Utawakamataaa....

CHORUS:- Diamond
Hivi Nyie Ma Mc's Mnachoimba kitu ganii, mara Bange mara Matusi sa ndo muziki ganii,

CHORUS:- Nay
Hii ni HIP HOP H.O.P, Ludboooy, Mwasisi wa burudanii, aah!, ukishatosha kutoa mapenzi kabane pua nyumbaniii

CHORUS:- Diamond
Hivi Nyie Ma Mc's Mnachoimba kitu ganii, mara Bange mara Matusi sa ndo muziki ganii,

CHORUS:- Nay
Hii ni HIP HOP H.O.P, Ludboooy, Mwasisi wa burudanii, aah!, ukishatosha kutoa mapenzi kabane pua nyumbaniii

NAY:- Muziki wenu Ushirikinaa, ndo Umetawala, Q-Chillah analalama, anasema umemloga, Mganga wako aliyekutoa umemkimbia hujamlipa, na Bila Skendo za magazeti basi husikikii....

DIAMOND:- Ahh!! me ni mti wenye matunda, milele siogopi kupigwa mawe, Ubaya wenu Kayumba, Elimu mmeitupa sandakarawee....

NAY:-  Halijanishawishii, Bongo Flava inanipa Kichefu che-fu, kwanza nyie malimbukeni wa umaarufu, Mnaleta maringo mpaka kwa mashabiki, Wabana pua nyie sio rizikii, Mnavaa nguo za dada zenu zinawabana majapa nyie makaka duu, Aaah!!, nyie watoto wa mchana mchanaa, DIAMOND anaingilia kati:- ''Mbona matusi bwana?'' Kwenye Shoo viuno mbele mbelee, ''Mbona unatutkanaa?'', Aah!! nyie watoto wa mchana mchanaa, ''Mbona matusi bwanaaa''?, Kwenye shoo viuno mbelembeleee, Tumewanyamazishaa, Braza Meni we vipi we bado unabishaa.....

DIAMOND:- Hata me nnamengi nayajuaaa, ila we mtemi utaanzisha utata, Michezo yenu kutoboa puaa, Bora ninyamaze usinipige Mbata...

CHORUS:- Diamond
Hivi Nyie Ma Mc's Mnachoimba kitu ganii, mara Bange mara Matusi sa ndo muziki ganii,

CHORUS:- Nay
Hii ni HIP HOP H.O.P, Ludboooy, Mwasisi wa burudanii, aah!, ukishatosha kutoa mapenzi kabane pua nyumbaniii

CHORUS:- Diamond
Hivi Nyie Ma Mc's Mnachoimba kitu ganii, mara Bange mara Matusi sa ndo muziki ganii,

CHORUS:- Nay
Hii ni HIP HOP H.O.P, Ludboooy, Mwasisi wa burudanii, aah!, ukishatosha kutoa mapenzi kabane pua nyumbaniii

DIAMOND:-  anamaliza kwa kicheko
Ha ha ha haaa, Umepanic Braza...

NAY:- Aaah! wapi nani kapanic, Acha Uwoga Dogoo...

WIMBO HUU UMEOMBWA NA Fatma Abdi wa Mwanza, Cuty Ashura wa Kinondoni, Dar, Magdalena Mmassy wa Arusha, na Maulid Ahmed wa Dar.
TUMA MAOMBI YAKO YA WIMBO WA BONGO FLAVA UUPENDAO, KATIKA EMAIL YAmuhidinuk@yahoo.co.uk

ANDIKA JINA LAKO KAMILI, MAHALA ULIPO NA WATU UNAOPENDA KUSHIRIKI NAO.

SAFU HII YA CHAGUO LA WIMBO LITAKUWA LIKITOKA KILA SIKU YA JUMATANO YA KILA WIKI KULINGANA NA MAOMBI YA WASOMAJI WA MTANDAO HUU.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni