Picha juu na chini ni Foleni ya magari ya takataka zaidi ya 30 yaliyokwama katika dampo la Pugu Kinyamwezi kwa takribani siku tatu kutokana na ubovu wa miundo mbinu huku taka zikiendelea kuoza ndani ya magari hayo na kusababisha harufu mbaya kwa wakazi wa maeneo hayo.
Katapila likiwa katika jitihada za kuchonga barabara ili angalau magari ya taka yaweze kufika eneo la dampo kuwamga taka.
Masela wakifurahia baada ya gari la taka lililokuwa limekwama kufanikiwa kupandisha kilima katika dampo hilo kuelekea kumwaga taka.
Wanafunzi wa shule ya msingi walipokutwa na camera yetu katika dampo hilo wakikatiza na kuzubaa zubaa eneo hilo wakati wa saa za shule.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni