MNENGUAJI Mahiri wa muziki wa dansi nchini, anayeshambulia na bendi ya Extra Bongo, Super Nyamwela, amekamilisha Song lake jipya linalokwenda kwa jina la Dullee Duvellee, linalopigwa katika mtindo wa Bongo Pop.
Akizungumza na mtandao wa www.sufianimafoto.com, Nyamwela, amesema kuwa Wimbo huo aliourekodia katika Studio za C91, zilizopo Kinondoni, amemshirikisha Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Muki kutoka katika Kundi la Makomandoo lililo chini ya THT.
Aidha alisema kuwa Msanii huyo aliyemshiriki ni yule anayetamba na Song lake kali ya Staili ya Kibega, ambao kwa pamoja katika wimbo huo wemefanya kazi ya kueleweka na inayomvutia kila mmoja atakayepata bahati ya kuusikiliza wimbo huo.
''Hivi sasa najipanga kuzindua staili yangu mpya ya Bongo Pop, inayokwenda na 'Swaga za Duvellee Duvellee' ambyo kwa maana halisi ya kiswahili cha Kitaa ni Shwari Shwari, na tayari wimbo huu nimeshausambaza katika Vituo mbalimbali vya Redio nchini na baadhi wameshaanza kuutendea haki kwa kuupiga na kuwapa raha wasikilizaji''. alisema Nyamwela
Pia Nyamwela amesema kuwa yupa katika maandalizi ya kurekodi Video ya Wimbo huo mwishoni mwa wiki hii katika Studio mpya za THT.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni