TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumatano, 15 Mei 2013

JAY DEE ATINGA MAHAKAMANI KINONDONI LEO KUFUATILIA KESI YAKE DHIDI YA CLOUDS


MWANAMUZIKI Mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kama 'Lady Jay Dee'  leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria katika kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi yake katika mahakama hiyo. 

Katika hati hiyo ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. 

Tuhuma za kesi hiyo zinatarajia kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu.

Jaydee aliwasili mahakamani hapo leo asubuhi akiwa ameongozana na mumewe Gadner G. Habash  na kuelekea chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni