TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Ijumaa, 31 Mei 2013

MTU MMOJA ATELEZA NA KUFARIKI DUNIA AKIJARIBU KUDANDIA DALADA ILALA BOMA LEO ASUBUHI

 'Innah Lillah Wainna Lillah Lajiun'', Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema asubuhi ya leo amefariki dunia baada ya kuteleza wakati alipokuwa ajijaribu kutaka kudandia usafiri wa Daladala maeneo ya Ilala Boma, Jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu huyo umeondolewa eneo hilo na kupelekwa Hospitali ya Amana. Marehemu huyo baada ya kuanguka na kupiga kichwa kwenye lami, alipasuka kichwa na kuvuja damu nyingi iliyopelekea umauti wake.
Hili ndilo Daladala alilokuwa akijaribu kudandia marehemu huyo.......

WABUNGE WA DRC WAMPONGEZA JK KWA MSIMAMO WAKE WA KUSAKA AMANI YA KUDUMU CONGO

Na VOA

Kufuatia wito wa rais Jakaya Kikwete kwa marais wa mataifa ya maziwa Makuu marais Paul Kagame, wa Rwanda, Joseph Kabila wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Yoweri Museveni wa Uganda, kuzungumza na makundi ya waasi yanayopambana na nchi zao, wabunge wa Kongo Kwenye taarifa yao ya pamoja iliyosomwa na mbunge Benjamin Mukulungu , wabunge hao wa Kivu Kusini na Kaskazini wameomba kuwe na mtazamo wa jumla wa viongozi wa kanda ya maziwa makuu na umoja wa mataifa ili kumaliza vita nchini Congo.
Wabunge wa Kivu wamepongeza msimamo wa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wa kutaka kuwe na mazungumzo kati ya serikali za Congo Rwanda na Uganda na makundi ya waasi wanayopingana nayo.
Wabunge wa Kivu wametaka pendekezo la Rais Kikwete ni lazima lipewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa ili kuwe na amani ya kudumu kwenye eneo hilo.
Mbunge wa upinzani Emerio Kunji kutoka jimbo la Kasai amesema amepanga kutoa hoja rasmi bungeni ili kuweko na azimio la bunge kuhusu msimamo ambao serikali ya Congo inatakiwa kuchukua kwa ajili ya kutatua mzozo wa Kivu.

Akisema “Rais wa Tanzania alichukua msimamo wa kijasiri wa kuonyesha kwamba mzozo wa maziwa makuu hauwezi kutambuliwa kwa njia ya kinafiki bali kupitia mtizamo ulio thabiti. Bunge letu ni lazima litoe shinikizo kwa serikali ili kuweko na mtizamo mpya wa ufumbuzi wa mzozo huo”.

NSSF MEDIA ALL STARS Vs WABUNGE LIVE ON STAR TV

 Kocha wa timu ya NSSF Media All Stars, Sanifu Lazaro akipimwa afya na Dk. Frida Francis kutoka Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda Dodo kupambana na timu ya Wabunge siku ya Jumamosi Juni Mosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Pambano hilo litaoneshwa Live kupitia Star Tv.
 Dk. Margreth Mtaki kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo akimpima afya mshambuliaji wa timu ya soka ya NSSF Media Kombaini, Maulid Kitenge kabla ya safari ya kwenda Dodoma kupambana na timu ya Wabunge. 
 Mchezaji wa timu ya Netiboli ya NSSF Media Kombani, Somoe Ng'tu akipimwa afya. 
 Majuto Omari akipimwa afya.

SUMITOMO CORPORATION FOR KINYEREZI POWER GENERATION

 The Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Dr. Servacius Likwelile and Sumitomo Corporation Senior Official signs a Memorandum of Understanding(MOU) for Kinyerezi 240 MW combined cycle power project at SUMITOMO Corporation Headquarters in Tokyo this morning. Witnessing the signing ceremony is President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and SUMITOMO Corporation President and CEO Mr.Kuniharu Nakamura.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete receives bouquet of  flowers shortly after he arrived at SUMITOMO Corporation Headquarters in Tokyo Japan for talks with senior corporation officials .Looking on is SUMITOMO Corporation President and CEO Mr.Kuniharu Nakamura. Photo by Freddy Maro

TANGAZO TANGAZO TANGAZO

Four Bedroom Villa in Prime location in the City available for immediate lease.
  • Fully Furnished
  • 24/7 Security, water, back up generator
  • Swimming Pool
  • Gym
  • Two Car Parkings.
Call Home Sweet Home Realtors for further details +255 784 786 455
Brand New Two/Three/Four Bedroom Apartments in Upanga, very centrally located Area. Close proximity to
  • Schools
  • Hospital
  • Shopping Stores
Available immediately. Fully Furnished with 24/7 Security, Water, backup Generator, Two elevators, Swimming pool, Gym and one car parking.
Call Home Sweet Home Realtors for further details +255 784 786 455
123Tanzania E-Shots

21,000+ Subscribers all over the Tanzania.
123Tanzania.com is the largest B2B online directory of Tanzania with more than 15,000 monthly visitors

Contact Us: English or Kiswahili +255 773 858 090, +255 22 213 3039

Email: info@123Tanzania.com
Copyright © 2013 123Tanzania, All rights reserved.
You are receiving this email from 123tanzania.com, Tanzania's largest Business portal. If you would like to unsubscribe from this list, simply click unsubscribe from the link below. Please note: unsubscribing from this list will only unsubscribe you from Newsletters E-Shots, it will not unsubscribe you from the Promo E-Shots.

Our mailing address is:
123Tanzania
Elia Complex
Zanaki Street
Dar Es Salaam 8758
Tanzania

Add us to your address book
unsubscribe from this list    update subscription preferences  

Jumatano, 29 Mei 2013

SUPER NYAMWELA AACHIA SONG JIPYA LA DUVELLEE DUVELLEE LA POP BONGO

MNENGUAJI Mahiri wa muziki wa dansi nchini, anayeshambulia na bendi ya Extra Bongo, Super Nyamwela, amekamilisha Song lake jipya linalokwenda kwa jina la Dullee Duvellee, linalopigwa katika mtindo wa Bongo Pop.
Akizungumza na mtandao  wa www.sufianimafoto.com, Nyamwela, amesema kuwa Wimbo huo aliourekodia katika Studio za C91, zilizopo Kinondoni, amemshirikisha Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Muki kutoka katika Kundi la Makomandoo lililo chini ya THT.

Aidha alisema kuwa Msanii huyo aliyemshiriki ni yule anayetamba na Song lake kali ya Staili ya Kibega, ambao kwa pamoja katika wimbo huo wemefanya kazi ya kueleweka na inayomvutia kila mmoja atakayepata bahati ya kuusikiliza wimbo huo.

''Hivi sasa najipanga kuzindua staili yangu mpya ya Bongo Pop, inayokwenda na 'Swaga za Duvellee Duvellee' ambyo kwa maana halisi ya kiswahili cha Kitaa ni Shwari Shwari, na tayari wimbo huu nimeshausambaza katika Vituo mbalimbali vya Redio nchini na baadhi wameshaanza kuutendea haki kwa kuupiga na kuwapa raha wasikilizaji''. alisema Nyamwela

Pia Nyamwela amesema kuwa yupa katika maandalizi ya kurekodi Video ya Wimbo huo mwishoni mwa wiki hii katika Studio mpya za THT.

*MISS SINZA/ MISS TANZANIA 2012-2013 BRIGIT ALFRED AWAFUNDA WAREMBO WA REDD'S MISS SINZA 2013

 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7,mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000. 
 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza. 
Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza. Picha zote na www.sufianimafoto.com

Jumanne, 28 Mei 2013

CCM YAFUNIKA MKUTANO WA LUDEWA,NJOMBE LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa CCM, kwenye Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoa wa Njombe, leo jioni. Kinana yupo katika ziara ya siku saba, kukagua utekelezaji wa ilani ya chama na kuzungumza na wananchi mkoani Njombe, amefuatana na Katiobu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Mei 28, 2013 katika Uwanja wa mpira mjini Ludewa mkoani Njombe. Picha na Bashir Nkoromo

MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MCHEZO WA CHESS KURINDIMA DAR JUNI 14

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Spicenet Tanzania Ltd, Vinay Choudary (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Chess yatakayoanza Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Michezo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea na mjumbe wa kamati ya chama cha chess, Emmanuel Mwaisumbe.
Raisi wa Chama cha Chess Tanzania (TACA), Geoffrey Mwanyika (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya Kimataifa ya mchezo wa Chess yatakayoanza Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Michezo katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chess Tanzania, Joe Anea na mjumbe wa kamati ya chama cha chess, Emmanuel Mwaisumbe.

STARS WATUA ADDIS ABABA SALAMA WAANZA KUJIFUA KUJIANDAA KUTOA DOZI

Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis.
Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.
Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0.
Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.

MSANII ALBERT MANGWAIR AFARIKI DUNIA AFRIKA YA KUSINI

Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Msanii mahiri wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwair, amefariki dunia, leo mchana akiwa nchini Afrika ya Kusini.

Chanzo cha habari hizi kimeeleza kwa njia ya SMS kutoka nchini Afrika ya Kusini, kimesema kuwa Msanii huyo amefariki wakati alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Hellena Joseph. 

Aidha Chanzo hicho kimesema kuwa msanii huyo alikuwa akiishi katika Ghetto Moja na Msanii M To The P, ambapo baadhi ya marafiki wa karibu wa msanii huyo walipofika katika geto hilo, walikuta tayari akiwa amefariki huku M To The P, akiwa amepoteza Fahamu ndani ya getho hilo. 
 
Pia Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa Ngwear Huko South Africa.  
Habari zilizo chini ya Kapeti zinasema kuwa Msanii huyo, Mangwair na mwenzake walikuwa wamejidunga madawa ya kulevya na kujioverdose, kiasi cha kuzima na kupoteza fahamu, ambapo wasanii hao walikuwa wakijiandaa kurejea nchini leo.

NBC WAMWAGA MISAADA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

Muuguzi  wa  Taasisi ya Saratani  ya Ocean Road  (ORCI) Sr.  Felista John (katikati aliyevaa gauni jeupe) akipokea msaada wa vyakula mbalimbali  kutoka Meneja Uendeshaji Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanaisha Ayosi, iliyotolewa na benki hiyo kitengo cha Operesheni ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo. Wengine ni wafanyakazi katika kitengo hicho.
 Mmoja wa wafanyakazi wa maofisa wa benki ya NBC, Lioba Massao (kushoto) akifanya maombezi kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  (ORCI) katika hafla ambayo benki hiyo kitengo cha operesheni kilikabidhi  msaada wa vyakula mbalimbali ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo na pia kumkabidhi msaada wa sabuni ya kufulia.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakibeba mizigo ya vyakula na mafuta ya kupikia tayari kuwakabidhi wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam kama sehemu ya juhudi za NBC katika kusaidia shughuli za jamii.

Ijumaa, 24 Mei 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UTOKOMEZAJI WA UGONJWA WA FISTULA, JIJINI DAR


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo leo, kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake, Patrick Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika Wodi ya wagonjwa wa Fistula, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
 Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT
 Baadhi ya wasichana waliokuwa wakiugua ugonjwa huo na kutibiwa katika Hospitali ya CCBRT, ambao kwa sasa wanapewa mafunzo ya kufanya kazi za mikono.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli za maadhimisho hayo.

RAIS KIKWETE ALIPOWAAPISHA MABALOZI WANNE NA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA SHERIA IKULU


 Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Modest Mero kuwa Balozi mpya wa Kidumu Umoja wa Mataifa (UN), nchini Geneva Uswis. Jumla ya Mabalozi wanne waliapishwa na Rais kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha sheria.
Rais Jakaya Kiwete Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Jaji Aloysius Mujulizi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, mbali na Mwenyekiti huyo wa Tume pia Rais aliwaapisha Mabolizi wanne kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali za nje.

Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Wilson Masilingi anaekwenda Uholanzi.
Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi ........
Rais Jakaya Kiwete akimwapisha Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Balozi Modest Mero.
 Rais Jakaya Kikwete akipiga picha ya pamoja na ndugu na jamaa wa Balozi Modest Mero Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa.
 Balozi Mero akiwa na ndugu zake Dalas (kushoto) na Mzirai.
 Balozi Modest Mero (kulia) akiwa na Michael Ley.
 Balozi Mero akipongezwa na Mpambe wa Rais (ADC to President) Kanali Kimario.
Balozi Mero akiwa na jamaa yake Richard Kasesela.

Jumatano, 22 Mei 2013

MTWARA KIMENUKA TENA, MMOJA APOTEZA MAISHA


Pichani ni moja ya mitaa ya Mtwara iliyoathirka na vurugu za leo, kwa kuchomwa matairi Barabarani, na kuharibu nyumba za wananchi na Ofisi za Serikali.
*******************************************
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
MTU mmoja amepoteza maisha, Wanne kujeruhiwa na 21 kutiwa mbaroni kufuatia vurugu zilizotokea leo Mkoani Mtwara baada ya Wananchi wa Mkoa huo kufunga baadhi ya mitaa na kuchoma matairi katika Barabara ya Zambia huku wakiharibu mali za wananchi na kuchoma Ofisi za Serikali pamoja na Nyumba ya Mwandishi wa Habari wa TBC.
Wananchi hao walianza kufanya vurugu hizo mara tu baada ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Bungeni mjini Dodoma leo, ambapo walikuwa wakipinga kile kilichoelezwa kutengwa kwa Bajeti ya Ujenzi wa Bomba la kusafirishia Gesi kutoka mkoani humo hadi Jijini Dar es Salaam.
Wananchi hao walianza vurugu hizo kwa kuvunja Daraja la Mikindani ambalo ni muhimu kwa mawasiliano kutoka Lindi na Dar kuingia Mtwara. 
 Aidha Imeelezwa kuwa katika harakati za kuongeza nguvu ya askari wa kudhibiti vurugu hizo, gari la Polisi limepinduka wakati likiwa katika mwendo mkali kuelekea Mtwara na kujeruhi baadhi ya askari.
Baadhi ya Ofisi zilizochomwa moto ni pamoja na Jengo la Ofisi ya CCM saba saba, Hotel Shengena, ambayo imeelezwa kuwa ni moja ya Hoteli waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwa ajili ya kuongeza nguvu ya Operation ya vurugu hizo zinazoendelea.
Pia Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  moto maeneo ya Shangani, huku wananchi hao wakirundika Mawe na Magogo makubwa katikati ya Barabara ili kuzuia magari ya askari kufanya kazi ya kutuliza vurugu hizo.
Kufuatia vurugu hizo katika hali isiyokuwa ya kawadida, Spika wa Bunge Anne Makinda leo ameahirisha Kikao cha Bunge ili kutoa nafasi kwa Uongozi wa Bunge kukutana na kujadili kwa kina vurugu hizo za Mtwara na kutafakari ili kupata suluhu ya vurugu hizo.

TZ ALL FEMALE STARS KIDOLE KIMOJA

Jumanne, 21 Mei 2013

KHADIJA SAID AIBUKA MISS UTALII TANZANIA


MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO  KATIKATI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM KUSHOTO NA MSHINDI WA TATU KULIA THELESIA KILOMO MISS UTALII VYUO VIKUU.
 MSHINDI WA TAJI LA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 HADIJA SAID MISS UTALII MOROGORO AKISHWA TAJI LA USHINDI NA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO
KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO
 KUTOKA KUSHOTO NI MISS UTALII KUTOKA MKOA WA KATAVI ASHA RAMADHANI ALIYE SHINDA NAFASI YA NNE, LUCY NOEL MISS UTALII DAR ES SALAAM ALIYESHINDA NAFASI YA PILI, MISS UTALII MOROGORO HADIJA SAID AMBAYE NDIYE MISS UTALII TANZANIA 2012/13, MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA TANGA LUTENI KANALI MSTAAFU CHIKU GALAWA,MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA BENDEGO ,MISS UTALII VYUO VIKUU THERESIA KILOMO NA MISS UTALII SINGIDA MWAKOMBO KESSY ALIYESHINDA NAFASI YA TANO

WASHIDI WA TANO BORA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI MKOA WA TANGA.