TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumatano, 12 Juni 2013

*REDD’S MISS TANZANIA YAZIDI KUNOGA

SAFARI ya kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu, inazidi kunoga kwani kesho (Ijumaa) na keshokutwa (Jumamosi), kutakuwa na vinyang’anyiro katika sehemu mbalimbali nchini.

Kazi kubwa inatarajiwa katika kumsaka Redd’s Miss Changombe, pale warembo zaidi ya 12 watakapopanda jukwaani, kumsaka mshindi kati yao.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Redd’s Miss Chang’ombe, kila kitu kimekamilika na shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa TCC Club, uliopo Chang’ombe, Dar es Salaam.

Burudani katika onyesho hilo ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 20,000 inatarajiwa kutolewa na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Pia kutakuwa na shindano la Redd’s Miss Iringa ambapo warembo watapanda jukwaani kusaka mwakilishi wa mkoa huo. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Ukumbi wa Highland.
Redd’s Miss Morogoro itafanyika Nashera Hotel, huku Redd’s Miss Mwanza ikiwa ndani ya Yacht Club na Redd’s Miss Central Zone, itafanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma.

Shindano hilo linatarajiwa kuendelea tena keshokutwa (Jumamosi) ambapo kutakuwa na Redd’s Miss Kilimanjaro na Redd’s Miss Kagera.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni