TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Alhamisi, 6 Juni 2013

MWILI WA MANGWEA ULIPOWASILI MOROGORO NJIA ZILIFUNGWA, MABASI YA ABIRIA YALIPIGWA 'STOP'

 Abiria waliokuwa wakisafiri na Basi la Aboud, wakiwa wametelemka chini baada ya magari yote yaliyokuwa yakielekea jiji Dar kutoka Morogoro kuzuiliwa kwa muda ili kupisha msafara wa magari yaliyokuwa yakiongozana na msiba wa Msanii Albert Mangwea, wakati ukiwasili mjini Morogoro leo jioni, ambapo umati wa watu ulijitokeza kuanzia Mikese kwa ajili ya kumpokea huku msafara huo ukidakwa na mapikipiki yapatayo kama 500 yaliyoanza kuongoza msafara huo kuelekea nyumbani kwa wazazi wa marehemu huku ulinzi ukiimarishwa zaidi kila kona ya mji huo wakati msafara huo ulipowasili.
 Askari wa usalama barabarani, akiongoza magari hayo wakati yakiwasili mjini Morogoro.
 Msafara huo ukipokelewa na Pikipiki maarufu kama Bodaboda zilizoanza kuongoza msafara huo kwa mwendo wa pole hadi nyumbani kwa marehemu.
 Sehemu ya pikipiki na umati wa watu waliokuwa pembezoni mwa barabara kushuhudia msafara huo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, KITALE, akisalimiana na mashabiki wake baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu. Msanii huyu mchana alitoka kali ya mwaka kwenye viwanja vya Leaders, baada ya kuibiwa simu na kumkamata mwizi wake na kisha kumpakia kwenye gari na kutokomea nae kusikojulikana.
 Msanii Afande Sele, akiwapokea wageni waliowasili na msafara huo.....
 Askari akitanga kiatu alichokiokota baada ya raia kusukumana eneo hilo wakigombea kuona jeneza lenye mwili wa marehemu.
Ulinzi pande hizi za nyumbani uliimarishwa kama hivi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni