TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumatano, 12 Juni 2013

MAAFISA WA POLISI WA BAVARIA UJERUMANI WATEMBELEA TRAFFIC

Mr. Gerd akipanda katika basi la ABOOD kuangalia namna shughuli za usafirishaji wa abiria katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo katika kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Jeshi la Polisi Nchini Ujerumani Jimbo la Bavaria. Aliyesimama chini ni Mr. Wolfgang Sommer akiwa na Mkuu wa Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni SSP. Ibrahim Mwamakula. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini DCP. Mohamed R. Mpinga akiwa eneo la taa za kuongozea magari za TAZARA akiwa na ugeni toka Bavaria Polisi Nchini Ujerumani akiwapa maelezo wageni wake namna askari wa usalama barabarani wanavyoongoza magari na changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani DCP. Mohammed Mpinga wa (pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa wageni waliofika Nchini kwa ziara ya kikazi kujionea namna kikosi cha usalama barabarani Nchini kinavyoendesha kazi zake katika kusimamia suala zima la usalama barabarani. Kutoka kulia kwa kamanda ni ACP. Nyambabe wa Polisi Makao Makuu DSM, Mr.wolfgang Sommer na Mr. Gerd Enkling kutoka Polisi Bavaria Ujerumani, wakifuatiwa na Mr. Conrad wa Hans siedel Foundation na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke ASP. Prackson Rugazia. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania DCP- Mohammed Mpinga (katikati) akiwa kituo kikuu cha mabasi Ubungo pamoja na wageni kutoka Polisi wa Bavaria Nchini Ujerumani waliofika Nchini kwa ziara ya kikazi. Hapa kamanda Mpinga akiwapa maelezo kuhusu utendaji kazi wa kila siku wa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani. Kulia kwa Kamanda ni Mr. Gerd Enkling (Colonel) wa Bavaria Police Ujerumani, Kushoto kwa Kamanda ni Mr.Walfgeng Sommer (Commissioner) Bavaria Police Ujerumani, nyuma ya Kamanda ni Mr. Conrad wa Hans Siedel Foundation na kulia kabisa ni ACP. Nyambabe wa Polisi Makao Makuu DSM. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni