TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU

Jumapili, 23 Juni 2013

SHOO YA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS TOUR 2013 KIKWETU KWETU, ILIVYOBAMBA MJINI DODOMA JANA

 Ommy Dimpozi, akiwasili uwanjani hapo....
 Ommy Dimpozi, akipozi kwa picha na madansa wake kabla ya kupanda jukwaani.
 Madansa wakisubiri kupanda jukwaani.
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel 5, Patrick Nyembela, akimhoji msanii Linex, kabla hajapanda kushambulia jukwaa.
 Sehemu ya umati wa mashabiki waliojitokeza kushuhudia shoo hiyo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Linex, akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour, 'Kiwetu Kwetu', lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, jana, KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Jumanne, 18 Juni 2013

*Skylight Band yazidi kuwachizisha mashabiki wake ndani ya Thai Village jijini Dar.

IMG_0959
Kikosi kazi cha Skylight Band kikisebeneka wakati wakitoa burudani kwa mashabiki wa kwenye show zao za kila Ijumaa ya mwisho wa wiki ndani ya Uwanja wa wa nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar.
IMG_0955
Minataka Mukanda ya Chuma chuma......Style mpya ya uchezaji ya Skylight Band. Pichani ni mashabiki wakijaribu miondoko hiyo.IMG_0918
Aneth Kushaba AK47 na Sam Mapenzi wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band.
IMG_0968
Mary Lucos akicheza na kuimba na mashabiki wa Skylight Band.
IMG_0974
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band aliyejaaliwa kipaji akionyesha ufundi wake wakusakata sebene huku wenzake wakimpigia makofi.
IMG_0973
Wakaka hawakukubali kushindwa na walijibu mapigo kwa wadada. Kanyaga twendeeeeee.
IMG_0975
Kiduku pia kilichezeka....Hapa chezea Skylight Band weweeee.... ndio habari ya mujini.
IMG_0924
Rapa Sony Masamba wa Skylight Band akiwajibika jukwaani.
IMG_0978
Utamu wa ngoma unapokolea inakuwa hivi.....Shabiki akinengua kwa Staili ya aina yake.
IMG_0935
Aneth Kushaba AK 47 katika hisia kali.
IMG_0942
Skylight Band ikiongozwa na Aneth Kushaba AK 47 wakitoa burudani kwa mashabiki wao.
IMG_0955
IMG_1015
Mduara nao ulihusika.
IMG_0990
Super Model wa ukweli kwenye pozi matata ndani ya nyumba.
IMG_0997
Wadau Victor Maginga (kulia) akishow love na mshikaji wake ndani ya Skylight Band.
IMG_0986
Warembo wa ukweeeeeh ndani ya nyumba.
IMG_1017
Kifaa kingine hicho kinaitwa Neema.
IMG_1007
Mdau askihow love.
IMG_1020
Mdau Dagma akishow love na Justin Ndege.
IMG_1028
Sam Mapenzi na Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo (asiyekubali anywe sumu ya panya) wakishow love mbele ya Camera yetu mara baada ya kutoa burudani kwa mashabiki wao....Njoo Ijumaa hii ujionee burudani ya Ukweli kutoka kwa vijana waliobarikiwa na kipaji kutoka kwa Muumba.

Jumapili, 16 Juni 2013

*''TAIFA STARS BADO TUPO TUPO KWANZA'', YAKUBALI KICHAPO CHA 4-2 TAIFA LEO

 Mshambuliaji wa Timu ya Ivory Cost,Traore Lacina, akiwania Mpira hewani na Beki wa Timu ya Taifa, Shomari Kapombe, wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2014, nchini Brazil uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Taifa Stars ililala kwa Mabao 4-2 dhidi ya Ivory Cost.
 Mshambuliaji Thomas Ulimwengu, 'Greda',  akimtoka beki wa Ivory Cost.
 Mtanange ulikuwa ni mzuri na wakuvutia, lakini...........
 Mshambuliaji wa Timu ya Ivory Cost,Yao Gervinho (kulia) akiwania mpira na Frank Domayo wakati wa Mchezo huo.

Jumatano, 12 Juni 2013

BLOG MPYA YA AFYA NJEMA; MAFANIKIO NA UTAJIRI

Soma kwa makini......

Pata majibu na maelezo ya maswali yafuatayo na matibabu ya njia rahisi kutoka blog ya Afya Njema; Mafanikio Na Utajiri (www.mtsimbe.blogspot.com)

·       Je Una Maumivi Ya Gouts (Viungo)?
·       Je Una Maumivu Ya Uti Wa Mgongo?
·       Je Una Tatizo la Kisukari?
·       Je Una Upara?
·       Je Ungependa Kuondoa Mabaka Mabaka Kwenye Ngozi?
·       Je, Nywele Zako Zinanyonyoka?
·       Je Una Fibroids Au Uvimbe Katika Kizazi?
·       Je Una Matatizo Ya Kushika Mimba?
·       Je Una Matatizo Na Siku Za Hedhi Au Maumivu?
·       Jinsi Ya Kupunguza Unene
·       Jinsi Ya Kuzuia Kumaliza Mapema
·       Je Jogoo Wako Hapandi Mtungi?
·       Je, Unapoteza Kumbukumbu?
·       Je, Ungependa Kuondoa Michirizi Katika Ngozi?
·       Jinsi Ya Kufanya Meno Yawe Meupe
·       Jinsi Ya Kuondoa Makunyanzi Ya Ngozi
·       Jinsi Ya Kufanya Matiti Yasimame (Yasilale)
·       Jinsi Ya Kuondoa Nywele Usoni
·       Je, Ungependa Kuwa Na Matiti Makubwa?
·       Je Macho Yako Hayaoni Vizuri?
·       Je, Una High Blood Pressure?
·       Je Una Allergies Na Kitu Chochote?
·       Jinsi Ya Kuondoa Vipele Vya Kunyoa Ndevu
·       Jinsi Ya Kuondoa Chunusi Usoni
·       Je Wewe Unakoroma Usiku Na Ungependa Uache?
Kwa maoni tuandikie: mtsimbe@gmail.com

*REDD’S MISS TANZANIA YAZIDI KUNOGA

SAFARI ya kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu, inazidi kunoga kwani kesho (Ijumaa) na keshokutwa (Jumamosi), kutakuwa na vinyang’anyiro katika sehemu mbalimbali nchini.

Kazi kubwa inatarajiwa katika kumsaka Redd’s Miss Changombe, pale warembo zaidi ya 12 watakapopanda jukwaani, kumsaka mshindi kati yao.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Redd’s Miss Chang’ombe, kila kitu kimekamilika na shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa TCC Club, uliopo Chang’ombe, Dar es Salaam.

Burudani katika onyesho hilo ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 20,000 inatarajiwa kutolewa na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Pia kutakuwa na shindano la Redd’s Miss Iringa ambapo warembo watapanda jukwaani kusaka mwakilishi wa mkoa huo. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Ukumbi wa Highland.
Redd’s Miss Morogoro itafanyika Nashera Hotel, huku Redd’s Miss Mwanza ikiwa ndani ya Yacht Club na Redd’s Miss Central Zone, itafanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma.

Shindano hilo linatarajiwa kuendelea tena keshokutwa (Jumamosi) ambapo kutakuwa na Redd’s Miss Kilimanjaro na Redd’s Miss Kagera.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

TOUR YA WASHINDI WA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2013 YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Music Tour unaotarajiwa kuanza wiki ijayo Mkoani Dodoma,wakati wa mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba na Muimbaji wa nyimbo za kizazi kipya, Diamod Platinam.
Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba.
Mwimbaji wa nyimbo za kizazi kipya,Kala Jeremier (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kutoka kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba, Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour ulifanyika Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam.
Waimbaji na washindi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa Kili Muzic Tour uliofanyika leo katika Hotel ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.

TUZO ZA FILAMU ZA STEPS KUTOLEWA JUMAMOSI JUNI 15

Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zitakaotolewa kwa wasanii sikuya Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, kulia ni Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba.
Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba (mwenye koti) akizungumzia udhamini wa kampuni yao katika tuzo za Steps Movie Award zilizopangwakufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl.

Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited Jumamosi itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania.

Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu.

Silondwa alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike, muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.

Silondwa alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.

Alisema kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.

“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.

Alisema kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps Solar pekee.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUPITIA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA, YAKABIDHI MSAADA WA KOMPYUTA KWA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA MJINI UNGUJA

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhi sehemu ya Compyuta 15, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu, kwa Kituo hicho cha Chwaka Computer Training Center. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la chwaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Uguja, (hayupo pichanio) wakati alipokua akizungumza baada ya makabidhiano hayo, alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Bilal.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhiwa sehemu ya Compyuta 15, na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula, ambapo Mkuu huyo wa mkoa wa Kusini unguja, alizikabidhi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, kwa niaba ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kwa ajili ya Kituo cha Chwaka Compyuter Training Center, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu Dkt. Bilal kwa kituo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni . Kushoto ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji, akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Chwaka mara baada ya makabidhiano ya Computer 15, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Makamu wa Rais Kwenye Kituo cha Chwaka Computer Training Center. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Chwaka Bw. Muhammed Ali (kushoto) ni Shekha wa Shehia ya Chwaka Bw. Msaraka Pinja na Mtendaji Mkuu wa Sayansi na Teknolojia Bw George Mulamula. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kituoni hapo. Picha na OMR.

MAAFISA WA POLISI WA BAVARIA UJERUMANI WATEMBELEA TRAFFIC

Mr. Gerd akipanda katika basi la ABOOD kuangalia namna shughuli za usafirishaji wa abiria katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo katika kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Jeshi la Polisi Nchini Ujerumani Jimbo la Bavaria. Aliyesimama chini ni Mr. Wolfgang Sommer akiwa na Mkuu wa Polisi Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni SSP. Ibrahim Mwamakula. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini DCP. Mohamed R. Mpinga akiwa eneo la taa za kuongozea magari za TAZARA akiwa na ugeni toka Bavaria Polisi Nchini Ujerumani akiwapa maelezo wageni wake namna askari wa usalama barabarani wanavyoongoza magari na changamoto wanazokutana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani DCP. Mohammed Mpinga wa (pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa wageni waliofika Nchini kwa ziara ya kikazi kujionea namna kikosi cha usalama barabarani Nchini kinavyoendesha kazi zake katika kusimamia suala zima la usalama barabarani. Kutoka kulia kwa kamanda ni ACP. Nyambabe wa Polisi Makao Makuu DSM, Mr.wolfgang Sommer na Mr. Gerd Enkling kutoka Polisi Bavaria Ujerumani, wakifuatiwa na Mr. Conrad wa Hans siedel Foundation na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke ASP. Prackson Rugazia. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania DCP- Mohammed Mpinga (katikati) akiwa kituo kikuu cha mabasi Ubungo pamoja na wageni kutoka Polisi wa Bavaria Nchini Ujerumani waliofika Nchini kwa ziara ya kikazi. Hapa kamanda Mpinga akiwapa maelezo kuhusu utendaji kazi wa kila siku wa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani. Kulia kwa Kamanda ni Mr. Gerd Enkling (Colonel) wa Bavaria Police Ujerumani, Kushoto kwa Kamanda ni Mr.Walfgeng Sommer (Commissioner) Bavaria Police Ujerumani, nyuma ya Kamanda ni Mr. Conrad wa Hans Siedel Foundation na kulia kabisa ni ACP. Nyambabe wa Polisi Makao Makuu DSM. Kikosi kilitembelewa tarehe 11/06/2013.